Na Andrew Chale, Bagamoyo. / ZanziNews
Baadhi ya wahitimu wa kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari ya Eagles wakiwa kwenye Mahafali yao ya 10, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba 6, Mjini Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Shule ya Sekondari ya Eagles ya Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani imefanya sherehe za Mahafali yake ya 10 na kuzindua rasmi mfumo mpya wa menejimenti ya shule ambao utasaidia wazazi kufuatilia maendeleao ya Watoto wao kwa ukaribu zaidi.
Akizundua mfumo huo sambamba na kutoa neno kwa wahitimu 71 wa kidato cha Nne wa shule hiyo mwishoni mwa wiki Oktoba 6,2018, Mgeni rasmi Mkaguzi na mdhibiti wa elimu bora Wilaya ya Bagamoyo Bwana. Davis Moye amewataka kuzingatia maadili sambamba na kujiandaa vyema kwa mitihani yao hiyo ya kuhitimu.
Akitoa neno kwa wahitimu hao: “Mjiandae vyema na mtafanya vizuri kwenye mitihani yenu. Pia niwapongeze kwa Eagles kuja na mfumo huu ambao utasaidia Wanafunzi na walimu kufanya mambo kifanisi zaidi.” Ameeleza Bwana Davis Moye.
Hata hivyo, amewataka Wazazi kufuatilia na kuwa karibu na watoto wao ili kubaini mapungufu kwa hatua ya kuyatatua.
Nae Mwenyekiti wa Bodi wa shule hiyo, Bi. Eva Fumbuka amejivunia kufanya vizuri kitaalum huku lengo kwa shule hiyo ni kuwa shule bora Kitaifa.
“Eagles mwaka 2006, ilikuwa ya kwanza kwa wavulana tupu kwa Wilaya ya Bagamoyo. Leo mahafali ya 10, matamanio yetu ni kufikia nafasi za juu zaidi kitaifa.
Eagles tumefanikiwa kutunukiwa vyeti vya shule bora kwa muda wa miaka tatu mfululizo na kwa kipindi cha miaka tano.
Pia ni mara ya tatu kupata mwanafunzi bora kwenye 10 bora ya kitaifa” alieleza Mwenyekiti huyo wa Bodi.
Kwa upande wake Meneja wa shule hiyo, Bwana. George Fumbuka amewashukuru wazazi kwa kuwaamini na hivyo wataendelea kufanyia kazi mapungufu huku wakitarajia kuanzisha kozi zaidi shuleni hapo ili kuendana na matakwa ya Nchi. “Kwa sasa tunakuja kufundisha lugha za Kifaransa, kiarabu na Kichina. Mafunzo ya kilimo, Kareti, vipaji na muziki vyote hivi vitapatikana hapa Eagles” alisema Meneja huyo wa shule.
Na Mtanzania Digital - October 8, 2018
Mgeni rasmi Mkaguzi na mdhibiti wa elimu bora Wilaya ya Bagamoyo Bwana. Davis Moye akiwa kwenye picha ya pamoja na wahitimu wa kidato cha Nne wa Shule ya Sekondari ya Eagles wakiwa kwenye Mahafali yao ya 10, yaliyofanyika mwishoni mwa wiki Oktoba 6,Mjini Bagamoyo, Mkoani Pwani.
Shule ya Sekondari ya Eagles ya Mjini Bagamoyo Mkoani Pwani, imefanya sherehe za mahafali yake ya 10 na kuzindua rasmi mfumo mpya wa Menejimenti ya Shule ambao utasaidia wazazi kufuatilia maendeleao ya watoto wao kwa ukaribu zaidi.
Akizundua mfumo huo sanjari na kutoa neno kwa wahitimu 71 wa kidato cha nne wa shule hiyo, mgeni rasmi Mkaguzi na Mdhibiti wa Elimu Bora Wilaya ya Bagamoyo, Davis Moye amewataka kuzingatia maadili na kujiandaa vyema kwa mitihani yao hiyo ya kuhitimu.
“Mjiandae vyema na mtafanya vizuri kwenye mitihani yenu, lakini pia nitumie nafasi hii kuwapongeza uongozi wa Eagles kuja na mfumo huu ambao utasaidia wanafunzi na walimu kufanya mambo kiufanisi zaidi,” amesema Moye.
Hata hivyo, amewataka wazazi kufuatilia na kuwa karibu na watoto wao ili kubaini mapungufu kwa hatua ya kuyatatua.
Naye Mwenyekiti wa bodi wa shule hiyo, Eva Fumbuka amejivunia kufanya vizuri kitaaluma na kuongeza kuwa lengo la shule hiyo ni kuwa shule bora kitaifa.
“Eagles mwaka 2006, ilikuwa ya kwanza kwa wavulana kwa Wilaya ya Bagamoyo, leo katika mahafali ya 10, matamanio yetu ni kufikia nafasi za juu zaidi kitaifa.
Tangazo la Sekondari ya Eagles. Watumie na marafiki zako!
Staff members from Eagles Secondary School in collaboration with Kawe Jogging Social Club, participated in the 5th Bagamoyo Historical Marathon, which was held on Sunday, 29th July 2018. Their participation in this event is part of their school's efforts to compliment government efforts in promoting sports and tourism in the country for the development of Bagamoyo town and for the benefit of the people of Tanzania at large.
Eagles Secondary School is Boarding School for Boys only located in the Nia Njema Area on the outskirts of Bagamoyo Township. Both the O-level and A-level Sections specialise in Science, Business and Arts subjects. The School has been in existence since 2006 and has during that time achieved notable successes. To push forward our development agenda, we need to fill the following positions. Competitive terms will be offered to suitable candidates, mostly performance-based:
The Board of Bahari Eagles Foundation Limited, owners of Eagles Secondary School in Bagamoyo, has appointed George Fumbuka, MBA FCCA, one of its Directors, to be School Manager as CEO of the School on its behalf effective from January 2018 for a 3-year period. He takes over from Francis Tabaro, another Director, who served as School Manager since 2012.
The Headmaster, Greyson Mhilu, stated: “Eagles celebrated its 12th Anniversary in January of this year, proudly having poured hundreds of O-level and A-level graduands into the Nation’s stock of human resources. These include doctors; bankers; engineers; and professional accountants. Two Alumni from our School recently graduated as Brokers of the Dar es Salaam Stock Exchange. This is a welcome development toward further successes”.