Jumamosi tarehe 27/Juni/2020 kulifanyika kikao maalumu cha kuzungumza na kidato cha sita ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza mtihani wa taifa. Kikao hicho kilihudhuriwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mama Eva Fumbuka,  mjumbe wa bodi ya shule Ndg. Peter Fumbuka pamoja na wafanyakazi wa shule ya Eagles.

Mambo mbalimbali yalizungumzwa na walimu ikiwa ni pamoja na kuwaasa wanafunzi kabla ya mtihani. Walimu waliwashukuru wanafunzi kwa kuonesha upekee na nidhamu nzuri katika kipindi hiki cha miaka miwili. Waliwaasa kuondoa hofu na kuwa kumtanguliza Mungu katika kipindi hiki cha mitihani.

Mkuu wa shule alizungumzia taratibu zote za mtihani wa taifa na kuwaasa wajiepushe na aina yoyote ya udanganyifu. Aliwataka wajiamini na kueleza imani yake kuwa ana imani kuwa wote watafaulu vizuri kwa kiwango cha daraja la kwanza. Alisisitiza kusameheana pale ambapo hatua zilichukuliwa kwa lengo zuri la kuwasaidia jambo ambalo lilihusisha adhabu mbalimbali.

Eagles high school hm anaongea 01

Mwenyekiti wa bodi ya shule alitoa ufafanuzi kuhusu umuhimu wa baba na mama katika jamii na hapa shuleni. Alimshukuru Rais wa Tanzania kwa hatua nzuri alizochukua kulikabili janga la ugonjwa wa Corona na kwa hatua ambazo zimepelekea tatizo kupungua na wanafunzi kuweza kurejea shuleni. Alisisitiza suala la kuondoa hofu na kumtanguliza Mungu kuwa ni muhimu sana katika kipindi hiki cha mitihani na kudhibiti ugonjwa wa Corona. Mkurugenzi aliwaasa wanafunzi kuwa raia wema mara watakapoondoka shuleni. Aliwakumbusha kuwa mabalozi wema wa shule hii na kuitangaza shule vizuri ili kuongeza idadi ya wanafunzi shuleni hapa.

Eagles high school mkurugenzi mama fumbuka anaongea 05

 

Katika kikao hicho wanafunzi walipewa pia vyeti vya kuhitimu na baadhi yao kupata vyeti kutokana na vipaji mbalimbali na uwezo mzuri walionesha ikiwemo ufaulu mzuri kitaaluma. Zoezi hilo la vyeti liliratibiwa na ofisi ya taaluma.

Eagles high school fumbuka jnr na mkurugenzi2 04

Eagles high school wanafunzi wanasikiliza3 07

Eagles high school wanafunzi wanasikiliza2 06