Jumatatu tarehe 1.05.2020 walimu wa Eagles High School walifanya semina kwa wanafunzi wa kidato cha sita kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujiandaa na mtihani wao wa taifa huku wakichukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19.

Mambo mengi yalizungumzwa ikiwa ni pamoja na kuondoa hofu ya mtihani, kujiamini, kujisomea kwa njia ya mjadala (group discussion), kumtanguliza Mungu na kutumia muda huu vizuri kufanya maandalizi. Hayo yameelezwa huku kila mmoja akisisitizwa kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa mapafu.

 

EaglesHS semina kidato cha VI 001

 

Tarehe 7 Machi 2020 kwenye shule ya sekondari ya Eagles kulifanyika mkutano wa wazazi, wafanyakazi pamoja na viongozi wa shule. Lengo la mkutano huu ni kujadili mambo mbalimbali yanayohusu shule ikiwa ni pamoja na maendeleo ya taaluma, nidhamu na ustawi wa wanafunzi. Mkutano  umekuwa mzuri na umeleta matokeo chanya.

mkutano wazazi Eagles HS 07 03 2020 2

 

Gallery: Academic staff, students and teachers