Shule ya sekondari Eagles iliyopo Bagamoyo inatangaza nafasi za kujiunga kidato cha tano 2020/2021.

Masomo ya awali ya kidato cha tano (Pre form five) yataanza 01.03.2020 kwa tahsusi za PCM, PCB, CBG, PMCs, CBCs, PCsG, PGM, CBA; Nyingine ni ECA, EGM, HGE, AgBE; pia zipo HGL, HKL,, HGK  na KLF.

Sifa ya kujiunga ni ufaulu wa mtihani wa taifa wa kidato cha 4 kuanzia daraja la I-III na alama za ufaulu ziwe kati ya 3 hadi 11 yaani AAA-CDD kwenye tahsusi.

Masomo ya Pre- form 5 yatatolewa bure! Mwanafunzi atatakiwa kuja na mahitaji yake binafsi na kulipia fedha ya kushika nafasi sh.300,000/- ambayo ni sehemu ya ada ya kidato cha tano.

Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni (Eagles), Msimbazi Centre duka no.9 na kwenye tovuti  ( www.eaglessecondary.com ). Kwa maelezo piga ( 0754303759, 0738719877,0738719875).