Mpango huo unaratibiwa na shirika la Opportunity Education ambalo linajukumu la kuandaa maudhui ya kufundishia kwa kutumia Tablet. Kwa kuanzia mpango huu umeanza kwa kidato cha Kwanza ambapo kila mwanafunzi na mwalimu wamepewa "Tablet" ambazo zimeunganishwa na mtandao wa Internet kutoka shirika la Vodacom Tanzania.

Eagles high school kompyuta combined 02

Walimu wa Masomo ndio wasimamizi wakuu wa ufundishaji na kuhakikisha kuwa wanafunzi wanajifunza na kutumia "tablet" hizo kwa malengo yaliyokusudiwa peke yake.

Awali shule ya Eagles ilizindua mpango mwingine wa kufundisha kwa kutumia "Tablet" aina ya iPad pamoja na kuanzisha somo la "Computer Science" kwa kidato cha tano na sita.