The Course runs for 12 weeks from 01/03/2021 to 31/5/2021. Though aimed at Boys who wish to join Eagles High School, it will also appeal to those waiting for their official NECTA results and possible Government placements later. We offer the course at TZS 500,000/=, refundable to those who join Eagles against their initial fees. We accept NECTA results so long as the Student has CDD in the chosen combination, but we reserve the right to suggest alternatives in consultation with the Parent.
Please download more information here
Wanafunzi hawa wamekuwa wakijifunza kwa njia ya mtandao (E-Learning) tangu mwanzoni mwa mwaka huu chini ya program inayoratibiwa kwa ushirikiano wa Opportunity Education na Vodacom Tanzania.
Hivi karibuni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilitoa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwenye Shule ya Sekondari ya EAGLES. Kwa mara nyingine tena, hii ilikuwa nafasi nzuri na muhimu kwa wanafunzi na wafanyakazi wote kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na majukumu makubwa ya Jeshi hili ambayo ni kuokoa Maisha na Mali katika majanga mbalimbali.
Aidha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifanya pia ukaguzi wa Kinga na Tahadhari dhidi ya majanga ya moto, na kutoa ushauri wa aina na namna ya uwekaji wa vifaa vya kinga na tahadhari.
Mechi ya kirafiki kati ya wafanyakazi na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita (A- Level). Mechi kama hizi ni muhimu Sana katika kujenga mahusiano mazuri ya miongoni mwa jumuiya ya Eagles.
Uongozi wa shule ya Eagles Hiugh School unayo furaha kuwatangazia kuwa umepokea matokeo mazuri ya mtihani wa Form 6 (ACSEE 2020) uliofanyika Juni/Julai 2020.
Baraza la mitihani la Taifa ( NECTA) limetoa matokeo ya kidato kidato cha sita mwaka 2020 kama ifuatavyo:
Kwa kidato cha sita: ACSEE_results_s2354_2020.pdf
Div: I- 13
II- 39
III- 31
IV- 03
0- 01
Katika matokeo hayo mwanafunzi Godfrey Assenga kutoka Eagles aliyekuwa akisoma tahsusi ya ECA amekuwa ni miongoni mwa wavulana kumi (10) Bora kitaifa kwa masomo ya biashara huku akishikilia Nafasi ya nane (8).
Mpango huo unaratibiwa na shirika la Opportunity Education ambalo linajukumu la kuandaa maudhui ya kufundishia kwa kutumia Tablet. Kwa kuanzia mpango huu umeanza kwa kidato cha Kwanza ambapo kila mwanafunzi na mwalimu wamepewa "Tablet" ambazo zimeunganishwa na mtandao wa Internet kutoka shirika la Vodacom Tanzania.