Hivi karibuni Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilitoa mafunzo ya kinga na tahadhari dhidi ya majanga ya moto kwenye Shule ya Sekondari ya EAGLES. Kwa mara nyingine tena, hii ilikuwa nafasi nzuri na muhimu kwa wanafunzi na wafanyakazi wote kujifunza mambo mbalimbali yanayohusiana na majukumu makubwa ya Jeshi hili ambayo ni kuokoa Maisha na Mali katika majanga mbalimbali.

Aidha Jeshi la Zimamoto na Uokoaji lilifanya pia ukaguzi wa Kinga na Tahadhari dhidi ya majanga ya moto, na kutoa ushauri wa aina na namna ya uwekaji wa vifaa vya kinga na tahadhari.