Wanafunzi hawa wamekuwa wakijifunza kwa njia ya mtandao (E-Learning) tangu mwanzoni mwa mwaka huu chini ya program inayoratibiwa kwa ushirikiano wa Opportunity Education na Vodacom Tanzania.
Mechi ya kirafiki kati ya wafanyakazi na wanafunzi wa kidato cha tano na cha sita (A- Level). Mechi kama hizi ni muhimu Sana katika kujenga mahusiano mazuri ya miongoni mwa jumuiya ya Eagles.
Mpango huo unaratibiwa na shirika la Opportunity Education ambalo linajukumu la kuandaa maudhui ya kufundishia kwa kutumia Tablet. Kwa kuanzia mpango huu umeanza kwa kidato cha Kwanza ambapo kila mwanafunzi na mwalimu wamepewa "Tablet" ambazo zimeunganishwa na mtandao wa Internet kutoka shirika la Vodacom Tanzania.
Jumamosi tarehe 27/Juni/2020 kulifanyika kikao maalumu cha kuzungumza na kidato cha sita ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza mtihani wa taifa. Kikao hicho kilihudhuriwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mama Eva Fumbuka, mjumbe wa bodi ya shule Ndg. Peter Fumbuka pamoja na wafanyakazi wa shule ya Eagles.
Mambo mbalimbali yalizungumzwa na walimu ikiwa ni pamoja na kuwaasa wanafunzi kabla ya mtihani. Walimu waliwashukuru wanafunzi kwa kuonesha upekee na nidhamu nzuri katika kipindi hiki cha miaka miwili. Waliwaasa kuondoa hofu na kuwa kumtanguliza Mungu katika kipindi hiki cha mitihani.
Mkuu wa shule alizungumzia taratibu zote za mtihani wa taifa na kuwaasa wajiepushe na aina yoyote ya udanganyifu. Aliwataka wajiamini na kueleza imani yake kuwa ana imani kuwa wote watafaulu vizuri kwa kiwango cha daraja la kwanza. Alisisitiza kusameheana pale ambapo hatua zilichukuliwa kwa lengo zuri la kuwasaidia jambo ambalo lilihusisha adhabu mbalimbali.
Shule ya sekondari Eagles itafunguliwa siku ya Jumapili tarehe 28.06.2020.
Wanafunzi wanaoanza kidato cha tano mwaka 2020 pia wataripoti siku hiyo kwa masomo yatakayoanza tarehe 29.06.2020.
Nafasi za kuhamia na kujiunga kidato cha tano bado zipo kwa tahsusi za PCM, PCB, PGM, CBG, PMC, CBC, ECA, HGE, EGM, KLF, HGL, HKL na HGK.
Wanafunzi wanatatakiwa kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa mapafu (Covid-19) kwa kuja na mahitaji k.m. vitakasa mikono (sanitizer) na barakoa (masks) za kutosha.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu hizi; 0738719877, 0738719870 na 0754303759.
The government has recently released selections of students to join form five studies, colleges and other institutions run by the government of the United Republic of Tanzania. 75 students from Eagles High School have been selected among 79 students, who completed form four last year. This outstanding performance equals to 95%.
We congratulate teachers, parents and students for the efforts, which brought about this great success.
We are inviting these students to come back to Eagles High School to do their form five studies.
Our school has highly dedicated staffs and is equipped with the best learning facilities and conducive environment for learning; These are among the factors that are playing a key role in the continuously best performances of our school. We offer the following combinations: PCM, PCB, PGM, CBG, CBC, PGM, PMC, ECA, HGE, EGM, KLF, HGL, HKL and HGK. Our school fees are affordable and can be paid in four installments.