Jumamosi tarehe 27/Juni/2020 kulifanyika kikao maalumu cha kuzungumza na kidato cha sita ikiwa ni siku mbili kabla ya kuanza mtihani wa taifa. Kikao hicho kilihudhuriwa na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi mama Eva Fumbuka, mjumbe wa bodi ya shule Ndg. Peter Fumbuka pamoja na wafanyakazi wa shule ya Eagles.
Mambo mbalimbali yalizungumzwa na walimu ikiwa ni pamoja na kuwaasa wanafunzi kabla ya mtihani. Walimu waliwashukuru wanafunzi kwa kuonesha upekee na nidhamu nzuri katika kipindi hiki cha miaka miwili. Waliwaasa kuondoa hofu na kuwa kumtanguliza Mungu katika kipindi hiki cha mitihani.
Mkuu wa shule alizungumzia taratibu zote za mtihani wa taifa na kuwaasa wajiepushe na aina yoyote ya udanganyifu. Aliwataka wajiamini na kueleza imani yake kuwa ana imani kuwa wote watafaulu vizuri kwa kiwango cha daraja la kwanza. Alisisitiza kusameheana pale ambapo hatua zilichukuliwa kwa lengo zuri la kuwasaidia jambo ambalo lilihusisha adhabu mbalimbali.
Shule ya sekondari Eagles itafunguliwa siku ya Jumapili tarehe 28.06.2020.
Wanafunzi wanaoanza kidato cha tano mwaka 2020 pia wataripoti siku hiyo kwa masomo yatakayoanza tarehe 29.06.2020.
Nafasi za kuhamia na kujiunga kidato cha tano bado zipo kwa tahsusi za PCM, PCB, PGM, CBG, PMC, CBC, ECA, HGE, EGM, KLF, HGL, HKL na HGK.
Wanafunzi wanatatakiwa kuchukua tahadhari ya Ugonjwa wa mapafu (Covid-19) kwa kuja na mahitaji k.m. vitakasa mikono (sanitizer) na barakoa (masks) za kutosha.
Kwa mawasiliano zaidi piga simu hizi; 0738719877, 0738719870 na 0754303759.
The government has recently released selections of students to join form five studies, colleges and other institutions run by the government of the United Republic of Tanzania. 75 students from Eagles High School have been selected among 79 students, who completed form four last year. This outstanding performance equals to 95%.
We congratulate teachers, parents and students for the efforts, which brought about this great success.
We are inviting these students to come back to Eagles High School to do their form five studies.
Our school has highly dedicated staffs and is equipped with the best learning facilities and conducive environment for learning; These are among the factors that are playing a key role in the continuously best performances of our school. We offer the following combinations: PCM, PCB, PGM, CBG, CBC, PGM, PMC, ECA, HGE, EGM, KLF, HGL, HKL and HGK. Our school fees are affordable and can be paid in four installments.
Jumatatu tarehe 1.05.2020 walimu wa Eagles High School walifanya semina kwa wanafunzi wa kidato cha sita kwa lengo la kuwajengea uwezo wa kujiandaa na mtihani wao wa taifa huku wakichukua tahadhari ya ugonjwa wa Covid-19.
Mambo mengi yalizungumzwa ikiwa ni pamoja na kuondoa hofu ya mtihani, kujiamini, kujisomea kwa njia ya mjadala (group discussion), kumtanguliza Mungu na kutumia muda huu vizuri kufanya maandalizi. Hayo yameelezwa huku kila mmoja akisisitizwa kuchukua tahadhari ya ugonjwa wa mapafu.
Tarehe 7 Machi 2020 kwenye shule ya sekondari ya Eagles kulifanyika mkutano wa wazazi, wafanyakazi pamoja na viongozi wa shule. Lengo la mkutano huu ni kujadili mambo mbalimbali yanayohusu shule ikiwa ni pamoja na maendeleo ya taaluma, nidhamu na ustawi wa wanafunzi. Mkutano umekuwa mzuri na umeleta matokeo chanya.
Shule ya sekondari Eagles iliyopo Bagamoyo inatangaza nafasi za kujiunga kidato cha tano 2020/2021.
Masomo ya awali ya kidato cha tano (Pre form five) yataanza 01.03.2020 kwa tahsusi za PCM, PCB, CBG, PMCs, CBCs, PCsG, PGM, CBA; Nyingine ni ECA, EGM, HGE, AgBE; pia zipo HGL, HKL,, HGK na KLF.
Sifa ya kujiunga ni ufaulu wa mtihani wa taifa wa kidato cha 4 kuanzia daraja la I-III na alama za ufaulu ziwe kati ya 3 hadi 11 yaani AAA-CDD kwenye tahsusi.
Masomo ya Pre- form 5 yatatolewa bure! Mwanafunzi atatakiwa kuja na mahitaji yake binafsi na kulipia fedha ya kushika nafasi sh.300,000/- ambayo ni sehemu ya ada ya kidato cha tano.
Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni (Eagles), Msimbazi Centre duka no.9 na kwenye tovuti ( www.eaglessecondary.com ). Kwa maelezo piga ( 0754303759, 0738719877,0738719875).