Mahafari hiyo ilifanyika tarehe 19/10/2019 na kuhudhuriwa na wazazi, watumishi pamoja na wageni mbalimbali. Pia mahafari ilihudhuriwa na wajumbe wa bodi ya shule wakiongoza na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Mama Eva Fumbuka.
Mgeni rasmi kwenye mahafari hii alikuwa Ndg. Kwangu Masalu Zabrone ambaye ni kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Utafiti na Machapisho wa Taasisi ya Elimu. Yeye alimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Dkt. Aneth Komba ambaye ndiye alitarajiwa kuwepo kwenye mahafari hiyo.
Katika mahafari hii kulifanyika pia maonesho ya kitaaluma (Academic exhibitions) ambayo yalikuwa kivutio kikubwa kwa wazazi pamoja na wageni mbalimbali.
Eagles ni shule ya sekondari ya wavulana, wote bweni, yenye Kidato cha 1 hadi cha 6. Imesajiliwa kama shule binafsi kwa namba S.2397 mwaka 2006 kutoa elimu ya sekondari kwa mitaala ya Tanzania. Shule yetu iko umbali wa kilometa 2 kutoka kituo kipya cha mabasi cha Bagamoyo karibu na kanisa kongwe Katoliki na Chuo cha ADEM upande wa magharibi.
MWAKA |
DIVISION I |
DIVISION II |
DIVISION III |
DIVISION IV / ZERO |
2015 |
4 |
5 |
11 |
0 |
2016 |
11 |
29 |
23 |
0 |
2017 |
7 |
35 |
54 |
0 |
2018 |
16 |
40 |
24 |
0 |
2019 |
16 |
56 |
36 |
0 |
Shule ina mazingira mazuri ya kitaaluma, walimu wa kutosha wenye sifa na mikakati mizuri ya kitaaluma yenye lengo la kumwezesha mwanafunzi kufaulu masomo yake. Aidha, Shule imeanzisha mfumo wa kufundisha kwa kutumia iPads za Apple zilizounganishwa na mtandao (Internet) ikiwa ni mkakati wa kuboresha ufundishaji ili uendane na teknolojia ya mawasiliano. Shule inayo masomo yote ya Sayansi, Sanaa, Biashara, Kilimo, Lugha na Kompyuta. Kwa Kidato cha 5 na cha 6 shule ina tahsusi zifuatazo:
Sanaa/Lugha: HGL (History, Geography, (English) Language); HGK (History, Geography, Kiswahili), HKL (History, Kiswahili, Language); KLF (Kiswahili, Language, French)
Biashara: ECA (Economics, Commerce, Accountancy); EGM (Economics, Geography, Mathematics); HGE (History, Geography, Economics); AgBE (Agriculture, Biology, Economics)
Sayansi: PCM (Physics, Chemistry, Mathematics); PCB (Physics, Chemistry, Biology); CBG (Physics, Biology, Geography); PMCs (Physics, Mathematics, Computer Science); CBCs (Chemistry, Biology, Computer Science); PCsG (Physics, Computer Science, Geography); PGM (Physics, Geography, Mathematics), CBA (Chemistry, Biology, Agriculture).
Shule ya sekondari Eagles imeanzisha mfumo wa kufundisha kwa kutumia iPad zilizounganishwa na internet. Mfumo huu unatajwa kuwa na manufaa mengi zaidi ikiwa ni pamoja na kumfanya mwanafunzi kulipenda somo hivyo kuongeza ufaulu. Pia mfumo huu unamuwezesha mwalimu kufundisha kwa kutumia mbinu shirikishi.
Wanafunzi wa kidato cha tano wakiwa darasani wakifuatilia somo la Computer Science kwenye Projector. Sekondari ya Eagles imeanzisha tahsusi mpya za PMCs, PCsG, na CBCs zenye somo jipya la Computer Science.
Wanafunzi wetu 63 waliomaliza kidato cha nne mwaka 2018 wamepata post mbalimbali kwenda kidato cha tano na vyuo mbalimbali vya serikali. Mchanganuo wa waliochaguliwa ni kama ifuatavyo: HGL- 11, PCM-9, PCB-1, HGE-8, PGM-2, HKL-2, EGM-6, ECA-7
Hali kadhalika wanafunzi wa Sekondari ya Eagles waliochaguliwa kwenda vyuo mbalimbali kwa stashahada na astashahada ni 17.
Tunatoa pongezi sana kwa wazazi na walimu kwa juhudi na ushirikiano mzuri waliounesha hadi kufikia mafanikio haya.
Picha mbalimbali za matukio ya mahafali ya kidato cha sita 2019 yaliyofanyika tarehe 06.05.2019 shuleni Eagles. Waliovalia fulana ni wahitimu wa kidato sita wakifurahia siku hii muhimu.
Meneja wa Sekondari ya Eagles Bw George Fumbuka akizungumza na wahitimu siku ya mahafali ya Form VI 2019