Top News

Tarehe 7 Machi 2020 kwenye shule ya sekondari ya Eagles kulifanyika mkutano wa wazazi, wafanyakazi pamoja na viongozi wa shule. Lengo la mkutano huu ni kujadili mambo mbalimbali yanayohusu shule ikiwa ni pamoja na maendeleo ya taaluma, nidhamu na ustawi wa wanafunzi. Mkutano  umekuwa mzuri na umeleta matokeo chanya.

mkutano wazazi Eagles HS 07 03 2020 2

 

Shule ya sekondari Eagles iliyopo Bagamoyo inatangaza nafasi za kujiunga kidato cha tano 2020/2021.

Masomo ya awali ya kidato cha tano (Pre form five) yataanza 01.03.2020 kwa tahsusi za PCM, PCB, CBG, PMCs, CBCs, PCsG, PGM, CBA; Nyingine ni ECA, EGM, HGE, AgBE; pia zipo HGL, HKL,, HGK  na KLF.

Sifa ya kujiunga ni ufaulu wa mtihani wa taifa wa kidato cha 4 kuanzia daraja la I-III na alama za ufaulu ziwe kati ya 3 hadi 11 yaani AAA-CDD kwenye tahsusi.

Masomo ya Pre- form 5 yatatolewa bure! Mwanafunzi atatakiwa kuja na mahitaji yake binafsi na kulipia fedha ya kushika nafasi sh.300,000/- ambayo ni sehemu ya ada ya kidato cha tano.

Fomu za kujiunga zinapatikana shuleni (Eagles), Msimbazi Centre duka no.9 na kwenye tovuti  ( www.eaglessecondary.com ). Kwa maelezo piga ( 0754303759, 0738719877,0738719875).

 

Baraza la mitihani la Taifa ( NECTA) limetoa matokeo ya kidato kidato cha pili na cha nne.

Kwa kidato cha pili: ftna_results_S2354-2019.pdf
Div:I- 09
      II-14
      III- 04
      IV- 03
Hakuna div 0.


Kwa kidato cha nne: csee_results_s2354-2019.pdf
Div: I- 17
       II- 46
       III- 14
       IV- 02
Hakuna div 0.

Wanafunzi 77 waliomaliza kidato cha nne wanna sifa ya kujiunga kidato cha tano mwaka huu huku wanafunzi 02 wakiwa wamepata div 4 ya point 26 ambayo wanaweza kupata nafasi ya kujiunga na vyuo mbalimbali.

Mahafari hiyo ilifanyika tarehe 19/10/2019 na kuhudhuriwa na wazazi, watumishi pamoja na wageni mbalimbali. Pia mahafari ilihudhuriwa na wajumbe wa bodi ya shule wakiongoza na mwenyekiti wa bodi ya wakurugenzi Mama Eva Fumbuka.

Mgeni rasmi  kwenye mahafari hii alikuwa Ndg. Kwangu Masalu Zabrone ambaye ni kaimu Mkurugenzi wa Idara ya Habari, Utafiti na Machapisho wa  Taasisi ya Elimu. Yeye alimwakilisha Mkurugenzi mkuu wa taasisi hiyo Dkt. Aneth Komba ambaye  ndiye alitarajiwa kuwepo kwenye mahafari  hiyo.

Katika mahafari hii kulifanyika pia maonesho ya kitaaluma (Academic exhibitions) ambayo yalikuwa kivutio kikubwa kwa wazazi pamoja na wageni mbalimbali.

EAGLES HighSchool 0161

Eagles ni shule ya sekondari ya wavulana, wote bweni, yenye Kidato cha 1 hadi cha 6. Imesajiliwa kama shule binafsi kwa namba S.2397 mwaka 2006 kutoa elimu ya sekondari kwa mitaala ya Tanzania. Shule yetu iko umbali wa kilometa 2 kutoka kituo kipya cha mabasi cha Bagamoyo karibu na kanisa kongwe Katoliki na Chuo cha ADEM upande wa magharibi.

TAALUMA:

MCHANGANUO WA MATOKEO YA KIDATO CHA SITA 2015-2019

MWAKA

DIVISION I

DIVISION II

DIVISION III

DIVISION IV / ZERO

2015

4

5

11

0

2016

11

29

23

0

2017

7

35

54

0

2018

16

40

24

0

2019

16

56

36

0

Shule ina mazingira mazuri ya kitaaluma, walimu wa kutosha wenye sifa na mikakati mizuri ya kitaaluma yenye lengo la kumwezesha mwanafunzi kufaulu masomo yake. Aidha, Shule imeanzisha mfumo wa kufundisha kwa kutumia iPads za Apple zilizounganishwa na mtandao (Internet) ikiwa ni mkakati wa kuboresha ufundishaji ili uendane na teknolojia ya mawasiliano. Shule inayo masomo yote ya Sayansi, Sanaa, Biashara, Kilimo, Lugha na Kompyuta. Kwa Kidato cha 5 na cha 6 shule ina tahsusi zifuatazo:

Sanaa/Lugha: HGL (History, Geography, (English) Language); HGK (History, Geography, Kiswahili), HKL (History, Kiswahili, Language); KLF (Kiswahili, Language, French)

Biashara: ECA (Economics, Commerce, Accountancy); EGM (Economics, Geography, Mathematics); HGE (History, Geography, Economics); AgBE (Agriculture, Biology, Economics)

Sayansi: PCM (Physics, Chemistry, Mathematics); PCB (Physics, Chemistry, Biology); CBG (Physics, Biology, Geography); PMCs (Physics, Mathematics, Computer Science); CBCs (Chemistry, Biology, Computer Science); PCsG (Physics, Computer Science, Geography); PGM (Physics, Geography, Mathematics), CBA (Chemistry, Biology, Agriculture).

Wanafunzi wa kidato cha Kwanza katika Shule ya sekondari Eagles wakifuatilia kwa makini somo la Kemia kwa kutumia iPad zilizounganishwa na internet.

Shule ya sekondari Eagles imeanzisha mfumo wa kufundisha kwa kutumia iPad zilizounganishwa na internet. Mfumo huu unatajwa kuwa na manufaa mengi zaidi ikiwa ni pamoja na kumfanya mwanafunzi kulipenda somo hivyo kuongeza ufaulu. Pia mfumo huu unamuwezesha mwalimu kufundisha kwa kutumia mbinu shirikishi.

Masomo ya Kemia kwa iPad EaglesHighSchool 1