Top News

Kwa mala nyingine shule ya sekondari ya Eagles imeshiriki kwenye mbio za Bagamoyo Marathon 2019. Mwaka huu watumishi wameshiriki kwa wingi zaidi ya mwaka jana. Lengo kubwa la mbio hizo ni kujenga umoja, kuimalisha afya ya watumishi, lakini kipekee sana ni kuitangaza shule ya kwa kuzingatia kuwa mbio hizo zinajumuisha watu wengi kutoka sehemu mbalimbali. Mgeni mashuhuri kwa mara nyingine alikuwa waziri wa maliasili na utalii Mh. Hamisi Kigwangala.

marathon2019 1

Sekondari ya Eagles imeanzisha tahsusi mpya za PMCs, PCsG, na CBCs zenye somo jipya la Computer Science.

FormV students Computer Science lesson2019 07 304
Wanafunzi wa kidato cha tano wakiwa darasani wakifuatilia somo la Computer Science kwenye Projector. Sekondari ya Eagles imeanzisha tahsusi mpya za PMCs, PCsG, na CBCs zenye somo jipya la Computer Science.

Uongozi wa shule ya Eagles Hiugh School unayo furaha kuwatangazia kuwa umepokea matokeo mazuri ya mtihani wa Form 6 (ACSEE 2019).

DIVISION I   16
DIVISION II  56
DIVISION III 36
DIVISION IV  1

JUMLA 109

necta a level 2019

 

ACSEE 2019 EXAMINATION RESULTS

Wanafunzi wetu 63 waliomaliza kidato cha nne mwaka 2018 wamepata post mbalimbali kwenda kidato cha tano na vyuo mbalimbali vya serikali. Mchanganuo wa waliochaguliwa ni kama ifuatavyo: HGL- 11, PCM-9, PCB-1, HGE-8, PGM-2, HKL-2, EGM-6, ECA-7

Hali kadhalika wanafunzi wa Sekondari ya Eagles waliochaguliwa kwenda vyuo mbalimbali kwa stashahada na astashahada ni 17.

Tunatoa pongezi sana kwa wazazi na walimu kwa juhudi na ushirikiano mzuri waliounesha hadi kufikia mafanikio haya.

headmaster eagles high school 2019 adam myombe

 

 

Kwa mara nyingine wanafunzi wa sekondari ya Eagles wamethibitisha uhodari wao sio tu katika masomo peke yake, bali pia hata katika Michezo ya Umiseta ngazi ya wilaya iliyofanyika siku ya Jumamosi tarehe 25/Mei/2019.

Mara hii michezo hii ngazi ya wilaya ilifanyika katika Shule ya sekondari Bagamoyo. Wanafunzi wengi wa sekondari ya Eagles walichaguliwa kushiriki michezo ya Umiseta ngazi ya mkoa itakayofanyika Kibaha.

Kwenye michezo hiyo wanafunzi wa sekondari ya Eagles waliambatana na  mratibu wa michezo Mwl. Sharif Mgulla ambaye ameshiriki kwa kiasi kikubwa kuanda timu hiyo. Kwenye mojawapo ya picha hapa chini ni mtu wa tatu kutoka kushoto aliyevalia t-shirt ya blue.

 Eagles High School Umiseta ngazi ya wilaya Bagamoyo 2019 1

Picha mbalimbali za matukio ya mahafali ya kidato cha sita 2019 yaliyofanyika tarehe 06.05.2019 shuleni Eagles. Waliovalia fulana ni wahitimu wa kidato sita wakifurahia siku hii muhimu.

mahafari kidato cha sita 06 05 2019 09

Meneja wa Sekondari ya Eagles Bw George Fumbuka akizungumza na wahitimu siku ya mahafali ya Form VI 2019